Makala Teule · Nguzo ya 4: Lugha za Kiafrika na Sarafu za Ndani
Hatua ya Kubadili Taswira Potofu na Kurejesha Kumbukumbu ya Taswira Iliyopotea
Imeandikwa na Hisham Kadri Ahmad · 15 Septemba 2025 · Imetafsiriwa na Hassan S. Ali · Chanzo: Qiraat Ifriqiya

Umoja wa Afrika ulitangaza, mwezi Agosti 2025, kuunga mkono rasmi kampeni ya “Sahihisheni Ramani”, iliyoanzishwa na baadhi ya mashirika ya kiraia kwa lengo la kutaka kupitishwa kwa ramani mpya inayoonyesha Afrika na nafasi yake ya kisiasa-kijiografia kwa ukubwa wake halisi, badala ya ramani ya zamani ya Mercator, ambayo inaonyesha bara hilo kwa namna inayopotosha na kutoa taswira isiyo sahihi.
Kampeni hii, inayoongozwa na mashirika mawili ya “Africa No Filter” na “Speak for Africa”, inaendana na juhudi za Umoja wa Afrika za kurekebisha taswira ya kiakili kuhusu bara hilo ambayo imejengeka kwa miongo mingi. Hatua hiyo inalenga, kwa hiyo, kuiwezesha Afrika kujitambulisha upya kwa mtazamo wake yenyewe, mbali na simulizi za Magharibi zinazolenga kulionyesha bara hilo kuwa dogo na kulisukuma pembeni, pamoja na kutoa mitazamo potofu kulihusu.
Ramani nyingi zinazotumiwa na mashirika ya kimataifa au taasisi za utafiti na elimu zinatokana na mchoro wa Mercator, uliobuniwa na mwanajiografia Gerard Mercator katika karne ya kumi na sita kwa ajili ya matumizi ya urambazaji na shughuli za ugunduzi wa Ulaya. Licha ya umaarufu mkubwa uliopata mchoro huu na kutumiwa kama msingi mkuu katika uchoraji wa ramani ya dunia kwa zaidi ya karne nne, mchoro huo unaonyesha upotoshaji mkubwa unaohusiana na ukubwa wa maeneo mbalimbali ya kijiografia ikilinganishwa na ukubwa wake halisi.
Bara la Afrika ni mfano dhahiri wa upotoshaji huo. Tunapotazama ramani iliyochorwa kwa kutumia mchoro wa Mercator, tunaona kwamba kisiwa cha Greenland, kilichopo upande wa kaskazini kabisa wa Bahari ya Atlantiki, kinaonekana kuwa na ukubwa unaokaribiana na bara la Afrika, ilhali kwa uhalisia Afrika ni kubwa kuliko Greenland kwa takribani mara 14. Vilevile, Amerika Kaskazini huonekana kuwa kubwa kuliko bara la Afrika, wakati kwa hakika ni dogo zaidi kwa kiasi kikubwa.
Sababu kuu ya upotoshaji huu haionekani kuwa ni ya makusudi, bali inatokana na ukweli kwamba katika mchoro huu wa kimviringo wa ramani, maeneo huonekana kuwa makubwa zaidi kadiri tunavyosogea kutoka Ikweta kuelekea kaskazini, katika upande wa Mzingo wa Aktiki, huku ukubwa wake ukipungua kadiri tunavyoelekea kusini.

Hata hivyo, upotoshaji uliosababishwa na mchoro wa Mercator na kugeuza taswira ya uhalisia haukuishia tu katika kuendeleza dhana potofu za kijiografia zilizodumu kwa zaidi ya karne nne, bali pia uliimarisha taswira potofu kuhusu Afrika kama bara dogo lililoko pembezoni, mbali na kitovu cha ustaarabu wa dunia. Taswira hiyo iliendana na kuunga mkono kile kinachotajwa kuwa usemi wa Magharibi wa kikoloni, ambao kwa muda mrefu uliitangaza Afrika kama eneo la mbali la kijiografia linalokaliwa na watu waliodaiwa kuwa wa kimaendeleo duni, wenye tofauti za urefu na maumbo ya miili, lakini wanaofanana katika ushenzi na ukatili wao. Yote hayo yalitumika kuhalalisha kampeni za kikoloni zilizomiminika barani Afrika, huku zikidai kwamba zilikuwa zikitekeleza jukumu la kibinadamu la kueneza ustaarabu na maendeleo katika bara hilo, katika mfumo wa dhana iliyojulikana wakati huo kama “Mzigo wa Mzungu” (The White Man’s Burden).
Katika mfumo wa juhudi za Waafrika zinazolenga kurejesha hadhi ya Afrika na kukomesha simulizi za kihistoria pamoja na mitazamo potofu ambayo imejengeka kuhusu bara hilo katika fikra za umma duniani, kutokana na ramani iliyopotoshwa inayoonyesha Afrika ikiwa ndogo sana kuliko ukubwa wake halisi, baadhi ya vyama na mashirika ya kiraia yameanzisha kampeni kubwa ya kusahihisha ramani ya Afrika. Hii inaonekana kuwa hatua muhimu ya kubadili mtazamo potofu uliopo kuhusu bara hilo, kupitia kuibua simulizi mbadala zinazosaidia kurejesha kumbukumbu ya taswira iliyopotea na kuimarisha taswira ya Afrika kama kitovu cha ustaarabu chenye ubunifu mwingi, huku kikikuza fursa za ukuaji na maendeleo.
Kampeni hii, inayoongozwa na mashirika mawili ya “Africa No Filter” na “Speak for Africa”, inatumia kaulimbiu “Sahihisheni Ramani (Correct the Map)”. Msingi wa kampeni hiyo ni kwamba mchoro wa Mercator hautoi tu uwakilishi usio wa haki wa nchi za Dunia ya Kusini kwa kuzionyesha kuwa ndogo ikilinganishwa na nchi za Kaskazini, bali pia huchangia kuimarisha mtazamo uliopo kwamba Afrika na nchi za Kusini zimetengwa na hazina uwezo wa kushindana na nchi za Kaskazini ambazo zinatawala ushawishi na nguvu.
Ili kuondokana na taswira hii potofu ambayo sasa imepitwa na wakati na haiakisi hali halisi ya dunia, kampeni hiyo inatoa wito wa kuangaliwa upya na kusahihishwa kwa ramani ya dunia kwa kuondoa matumizi ya mchoro wa Mercator na badala yake kupitisha Mchoro wa Dunia Iliyolingana (The Equal Earth Projection). Kampeni hiyo pia inatoa wito wa kuingizwa kwa ramani mpya ya Afrika katika mitaala na programu za elimu.
Lengo la Mchoro wa Dunia Iliyolingana (The Equal Earth Projection), ambao ni aina ya mchoro wenye umbo la nusu-silinda uliotengenezwa mwaka 2018 na Bernhard Jenny kutoka Chuo Kikuu cha Monash nchini Australia, Tom Patterson kutoka Huduma ya Hifadhi za Taifa ya Marekani, pamoja na Bojan Savric, ni kuonyesha nchi zilizoendelea za Kaskazini pamoja na nchi zinazoendelea za Kusini, zikiwemo nchi za Afrika, kwa ukubwa unaolingana na ukubwa wao halisi bila upotoshaji. Hili hufanyika kwa kuonyesha mipaka na maumbo ya mabara kwa njia ya kuvutia, yenye uwiano na inayoeleweka kwa urahisi.¹
Umoja wa Afrika umetangaza kuunga mkono kikamilifu kupitishwa kwa Mchoro wa Dunia Iliyolingana, huku ukizitaka taasisi za kimataifa kuachana na ramani ya Mercator. Aidha, Umoja huo uliwasilisha ombi rasmi kwa Kamati ya Umoja wa Mataifa inayohusika na masuala ya ramani (UN-GGIM), iliyo chini ya Umoja wa Mataifa, ili kupitisha ramani hiyo mbadala kwa lengo la kurekebisha taswira ya kiakili ya Afrika duniani.
Kuhusiana na suala hilo, Salma Malika Haddadi, Naibu Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika, alisema kwamba suala hili halihusu ramani tu, bali linahusu taswira ya kiakili ambayo imejengeka kwa miongo kadhaa. Alisisitiza kwamba Umoja wa Afrika unaunga mkono mpango huu kwa sababu unaendana na lengo lake la kurejesha Afrika katika nafasi yake inayostahili katika medani ya kimataifa, wakati ambapo wito wa kutaka fidia kutokana na kipindi cha ukoloni na utumwa unazidi kuongezeka.²

Msimamo huu unaonyesha namna Umoja wa Afrika unavyotambua umuhimu wa ramani, si kwa sababu tu ni chombo cha kuonyesha mwelekeo na maeneo, bali pia kama hati ya taswira inayounda mahusiano ya nguvu na kuathiri namna dunia inavyoifikiria. Kwa hiyo, kuungwa mkono na Umoja wa Afrika kwa madai ya kupitishwa kwa Mchoro wa Dunia Iliyolingana kunaweza kutazamwa kama hatua inayolenga kuandika upya historia ya Afrika kwa kutumia lugha mpya ya taswira, kwa matumaini ya kuondokana na mfumo wa taswira potofu unaolifungamanisha bara la Afrika na umaskini, magonjwa ya milipuko na migogoro ya silaha, na badala yake kuonyesha nyanja nyingine zinazosisitiza nguvu ya Afrika katika demografia na uchumi.³
Inaweza kusemwa kwamba juhudi za kupitisha au kuidhinisha ramani mpya inayoonyesha Afrika na nchi za Dunia ya Kusini kwa ukubwa wake halisi zinawakilisha hatua ya kiishara ya kurejesha hadhi ya watu wa Afrika miongoni mwa mataifa. Ramani ambayo Waafrika na Umoja wa Afrika wanaitaka ni sehemu ya madai ya kurejeshwa kwa haki na kushughulikiwa kwa dhuluma za kihistoria ambazo nchi na watu wa bara hili walikumbana nazo kwa zaidi ya karne moja mikononi mwa tawala za kikoloni za Ulaya. Aidha, hatua hii, licha ya kuwa ya kiishara, inaweza kuimarisha hisia za umoja na utambulisho miongoni mwa watu wa bara hili, na kuonyesha uwezo wa Afrika wa kujitengenezea maono yake na kuunda mitazamo yake kuhusu yenyewe, badala ya kutegemea yale ambayo wengine wanataka iwe au wanavyoichora na kuielezea.
Afrika si bara lililotengwa au lililo mbali na kitovu cha nguvu za kimataifa kama linavyoonyeshwa na ramani ya Mercator. Kinyume chake, takwimu za hali halisi zinaonyesha kwamba eneo la Afrika ni sawa na jumla ya maeneo ya Ulaya, Marekani, China na Japan kwa pamoja. Bara hili lina wakazi zaidi ya bilioni moja na linajumuisha nchi 54, huku likiwa na utajiri mkubwa wa maliasili na madini ya kimkakati yaliyomo ndani ya ardhi yake, ambayo yanaimarisha nafasi yake kama mshiriki mwenye ushawishi katika siasa za kimataifa.
Hata hivyo, safari ya kutafuta ramani mpya itakayoirejeshea Afrika uzito wake halisi duniani bado ni kazi ngumu, kwa kuwa ni sehemu ya mwendelezo wa mapambano mapana zaidi ambayo bara hili linaendelea nayo ili kuwasilisha simulizi yake yenyewe na kuondokana na simulizi ya kikoloni iliyotawala kwa karne nyingi. Lakini mafanikio ya Afrika katika jukumu hili, bila shaka, yataimarisha mtaji wake wa kidiplomasia na kiuchumi, ambao unaweza kutumiwa na kuendelezwa kwa njia chanya ili kuinua hadhi ya bara la Afrika miongoni mwa mataifa.⁴
Kwa hitimisho, inaweza kusemwa kwamba kuungwa mkono na Umoja wa Afrika kwa kupitishwa kwa ramani mpya inayoonyesha bara hilo kwa ukubwa wake halisi kuna maana pana za kisiasa. Kwa upande mmoja, mpango huu unaonyesha msisitizo wa taasisi hiyo ya kikanda kuhusu uhuru wa kimkakati wa bara na juhudi zake za kuvuka kipindi cha utegemezi wa kisiasa. Kwa upande mwingine, unafungua tena uwezekano wa mjadala kuhusu masuala yaliyopo kwa muda mrefu yanayohusiana na fidia zinazodaiwa kustahili kutolewa kwa nchi za Afrika kutokana na utumwa na ukoloni.
Hata hivyo, mwelekeo huu wa Umoja wa Afrika unahitaji utashi wa kweli wa kisiasa ili kuugeuza kuwa uhalisia. Hii ni kwa sababu si rahisi kutarajia serikali, mashirika na jumuiya za kimataifa, pamoja na vyombo vya habari duniani, kukubali kwa urahisi mpango huu unaolenga kubadilisha ramani ambayo imetumika kwa karne kadhaa na kuweka nyingine ambayo imetengenezwa katika miaka michache iliyopita.
1أعلن الاتحاد الإفريقي، في أغسطس 2025م، دعمه رسميًّا لحملة “صحِّحوا الخريطة”؛ التي أطلقتها بعض المُنظمات المدنية للمُطالبة باعتماد خريطة جديدة تُظهر إفريقيا ومكانتها الجيوسياسية بحجمها الفعلي بدلًا من خريطة ميركاتور Mercator القديمة التي تعكس صورة القارة بطريقة مُضلّلة ومشوَّهة.
1Umoja wa Afrika ulitangaza, mwezi Agosti 2025, kuunga mkono rasmi kampeni ya “Sahihisheni Ramani”, iliyoanzishwa na baadhi ya mashirika ya kiraia kwa lengo la kutaka kupitishwa kwa ramani mpya inayoonyesha Afrika na nafasi yake ya kisiasa-kijiografia kwa ukubwa wake halisi, badala ya ramani ya zamani ya Mercator, ambayo inaonyesha bara hilo kwa namna inayopotosha na kutoa taswira isiyo sahihi.
2تأتي هذه الحملة، التي تقودها منظمتا “إفريقيا بلا تنميط Africa No Filter”، و”تحدّث لأجل إفريقيا Speak for Africa”، متناغمةً مع جهود الاتحاد الإفريقي الذي يطمح إلى تصحيح الصورة الذهنية عن القارة التي ترسَّخت لعُقود طويلة، وبالتالي إعادة تعريف إفريقيا لذاتها بعيدًا عن السرديات الغربية التي تسعى إلى تقزيم القارة وتهميشها، وطرح تصوُّرات مُضللة بشأنها.
2Kampeni hii, inayoongozwa na mashirika mawili ya “Africa No Filter” na “Speak for Africa”, inaendana na juhudi za Umoja wa Afrika za kurekebisha taswira ya kiakili kuhusu bara hilo ambayo imejengeka kwa miongo mingi. Hatua hiyo inalenga, kwa hiyo, kuiwezesha Afrika kujitambulisha upya kwa mtazamo wake yenyewe, mbali na simulizi za Magharibi zinazolenga kulionyesha bara hilo kuwa dogo na kulisukuma pembeni, pamoja na kutoa mitazamo potofu kulihusu.
3تعود معظم الخرائط المُعتمَدة مِن قِبَل المُنظمات الدولية أو المؤسسات البحثية والتعليمية إلى إسقاط ميركاتور، الذي ابتكره عالم الجغرافيا جيرارد ميركاتور Gerard Mercator في القرن السادس عشر لخدمة أغراض الملاحة وحركة الكشوف الأوروبية، وعلى الرغم من الشهرة الواسعة التي حظي بها هذا الإسقاط واعتماده معيارًا رئيسيًّا في رسم الخريطة العالمية لأكثر من أربعة قرون؛ إلا أنَّ هذا الإسقاط يُظهر تشوُّهات واضحة تتعلق بحجم الأقاليم الجغرافية مقارنةً بحجمها الحقيقي.
3Ramani nyingi zinazotumiwa na mashirika ya kimataifa au taasisi za utafiti na elimu zinatokana na mchoro wa Mercator, uliobuniwa na mwanajiografia Gerard Mercator katika karne ya kumi na sita kwa ajili ya matumizi ya urambazaji na shughuli za ugunduzi wa Ulaya. Licha ya umaarufu mkubwa uliopata mchoro huu na kutumiwa kama msingi mkuu katika uchoraji wa ramani ya dunia kwa zaidi ya karne nne, mchoro huo unaonyesha upotoshaji mkubwa unaohusiana na ukubwa wa maeneo mbalimbali ya kijiografia ikilinganishwa na ukubwa wake halisi.
4وتبرُز القارة الإفريقية كمثال واضح على هذه التشوُّهات؛ فعند مطالعة الخريطة المُصمَّمة طبقًا لإسقاط ميركاتور، نلاحظ أنَّ جزيرة جرينلاند الواقعة أقصى شمال المُحيط الأطلسي تبدو في حجم مقارب لقارة إفريقيا في حين أنَّ هذه الأخيرة أكبر منها بنحو 14 مرةً، كذلك تبدو أمريكا الشمالية أكبر من القارة الإفريقية، بينما هي في الواقع أصغر منها بكثير.
4Bara la Afrika ni mfano dhahiri wa upotoshaji huo. Tunapotazama ramani iliyochorwa kwa kutumia mchoro wa Mercator, tunaona kwamba kisiwa cha Greenland, kilichopo upande wa kaskazini kabisa wa Bahari ya Atlantiki, kinaonekana kuwa na ukubwa unaokaribiana na bara la Afrika, ilhali kwa uhalisia Afrika ni kubwa kuliko Greenland kwa takribani mara 14. Vilevile, Amerika Kaskazini huonekana kuwa kubwa kuliko bara la Afrika, wakati kwa hakika ni dogo zaidi kwa kiasi kikubwa.
5والسبب الرئيس في هذه التشوُّهات لا يبدو متعمدًا، وإنما يرجع إلى أنَّ هذا الإسقاط الأسطواني للخرائط تبدو فيه الأجسام أكبر حجمًا كلما تجاوزنا خط الاستواء شمالًا باتجاه الدائرة القطبية الشمالية، بينما يصغر حجمها كلما اتجهنا جنوبًا.
5Sababu kuu ya upotoshaji huu haionekani kuwa ni ya makusudi, bali inatokana na ukweli kwamba katika mchoro huu wa kimviringo wa ramani, maeneo huonekana kuwa makubwa zaidi kadiri tunavyosogea kutoka Ikweta kuelekea kaskazini, katika upande wa Mzingo wa Aktiki, huku ukubwa wake ukipungua kadiri tunavyoelekea kusini.

6غير أنَّ هذه التشوُّهات التي أحدثها إسقاط ميركاتور وحرَّفت الواقع، لم تُكرّس فقط مغالطات جغرافية دامت لأكثر من أربعة قرون، بل عزَّزت أيضًا صورة نمطية مُضلّلة بشأن إفريقيا بوصفها قارةً صغيرةً تقع على الأطراف بعيدًا عن مركز الحضارة العالمي، وهي الصورة التي تتسق وتخدم الخطاب الغربي “الاستعماري” الذي لطالما كان يُرِّوج لإفريقيا بوصفها بقعةً جغرافيةً نائيةً، يقطنها سكان بدائيون يتفاوتون في أطوالهم وأجسامهم ويتشابهون في همجيتهم وبربريتهم، وكل ذلك من أجل تبرير الحملات الاستعمارية التي تدافعت على إفريقيا، زاعمةً أنها تحمل على عاتقها مهمةً إنسانية تتمثل في نشر الحضارة والتقدم في ربوع القارة السمراء، في إطار ما عُرف حينها بـ”عبء الرجل الأبيض”.
6Hata hivyo, upotoshaji uliosababishwa na mchoro wa Mercator na kugeuza taswira ya uhalisia haukuishia tu katika kuendeleza dhana potofu za kijiografia zilizodumu kwa zaidi ya karne nne, bali pia uliimarisha taswira potofu kuhusu Afrika kama bara dogo lililoko pembezoni, mbali na kitovu cha ustaarabu wa dunia. Taswira hiyo iliendana na kuunga mkono kile kinachotajwa kuwa usemi wa Magharibi wa kikoloni, ambao kwa muda mrefu uliitangaza Afrika kama eneo la mbali la kijiografia linalokaliwa na watu waliodaiwa kuwa wa kimaendeleo duni, wenye tofauti za urefu na maumbo ya miili, lakini wanaofanana katika ushenzi na ukatili wao. Yote hayo yalitumika kuhalalisha kampeni za kikoloni zilizomiminika barani Afrika, huku zikidai kwamba zilikuwa zikitekeleza jukumu la kibinadamu la kueneza ustaarabu na maendeleo katika bara hilo, katika mfumo wa dhana iliyojulikana wakati huo kama “Mzigo wa Mzungu” (The White Man’s Burden).
7في إطار الجهود الإفريقية الرامية إلى إعادة الاعتبار لإفريقيا ووضع حدٍّ للسرديات التاريخية والتصوُّرات المغلوطة التي تكوَّنت عنها في أذهان الرأي العام العالمي، انطلاقًا من الخريطة المشوَّهة التي تُظهر إفريقيا بحجم أقل بكثير من حجمها الطبيعي، أطلقت بعض الجمعيات والمُنظمات المدنية حملةً موسَّعة لتصحيح خريطة إفريقيا كخطوة ضرورية لتغيير النظرة النمطية السائدة عنها من خلال طرح سرديات مُغايرة تُسهم في استعادة الذاكرة البصرية المفقودة، وتُعزّز صورة القارة باعتبارها موطنًا حضاريًّا يزخر بالابتكار ويُعزّز فرص النمو والتقدم.
7Katika mfumo wa juhudi za Waafrika zinazolenga kurejesha hadhi ya Afrika na kukomesha simulizi za kihistoria pamoja na mitazamo potofu ambayo imejengeka kuhusu bara hilo katika fikra za umma duniani, kutokana na ramani iliyopotoshwa inayoonyesha Afrika ikiwa ndogo sana kuliko ukubwa wake halisi, baadhi ya vyama na mashirika ya kiraia yameanzisha kampeni kubwa ya kusahihisha ramani ya Afrika. Hii inaonekana kuwa hatua muhimu ya kubadili mtazamo potofu uliopo kuhusu bara hilo, kupitia kuibua simulizi mbadala zinazosaidia kurejesha kumbukumbu ya taswira iliyopotea na kuimarisha taswira ya Afrika kama kitovu cha ustaarabu chenye ubunifu mwingi, huku kikikuza fursa za ukuaji na maendeleo.
8هذه الحملة، التي تقودها مُنظمتا “إفريقيا بلا تنميط Africa No Filter” و”تحدث لأجل إفريقيا”، ترفع شعار “صحِّحوا الخريطة Correct the Map” من منطلق أنَّ إسقاط ميركاتور لا يُقدّم فقط تمثيلًا غير عادل لدول الجنوب العالمي بتصويره لها أصغر حجمًا مقارنةً بدول الشمال، بل يُسهم في ترسيخ الانطباع السائد بأنَّ إفريقيا ودول الجنوب مُهمَّشة ولا ترقى إلى منافسة دول الشمال التي تحتكر النفوذ والقوة.
8Kampeni hii, inayoongozwa na mashirika mawili ya “Africa No Filter” na “Speak for Africa”, inatumia kaulimbiu “Sahihisheni Ramani (Correct the Map)”. Msingi wa kampeni hiyo ni kwamba mchoro wa Mercator hautoi tu uwakilishi usio wa haki wa nchi za Dunia ya Kusini kwa kuzionyesha kuwa ndogo ikilinganishwa na nchi za Kaskazini, bali pia huchangia kuimarisha mtazamo uliopo kwamba Afrika na nchi za Kusini zimetengwa na hazina uwezo wa kushindana na nchi za Kaskazini ambazo zinatawala ushawishi na nguvu.
9ولتجاوز هذه الصورة المُضللة التي أصبحت من الماضي ولا تعكس مُعطيات الواقع، تدعو الحملة إلى إعادة النظر في خريطة العالم وتصحيحها من خلال استبعاد إسقاط ميركاتور، واعتماد إسقاط الأرض المتساوية بدلًا منه، كما تدعو الحملة كذلك إلى إدراج الخريطة الجديدة لإفريقيا في المناهج والمُقررات التعليمية.
9Ili kuondokana na taswira hii potofu ambayo sasa imepitwa na wakati na haiakisi hali halisi ya dunia, kampeni hiyo inatoa wito wa kuangaliwa upya na kusahihishwa kwa ramani ya dunia kwa kuondoa matumizi ya mchoro wa Mercator na badala yake kupitisha Mchoro wa Dunia Iliyolingana (The Equal Earth Projection). Kampeni hiyo pia inatoa wito wa kuingizwa kwa ramani mpya ya Afrika katika mitaala na programu za elimu.
10ويهدف إسقاط الأرض المتساويةThe Equal Earth ، وهو إسقاط شبه أسطواني تم تطويره عام 2018م مِن قِبَل كلٍّ من “برنارد جيني “Bernhard Jenny من جامعة موناش الأسترالية و”توم باترسون Tom Patterson” من دائرة المتنزهات الوطنية الأمريكية، وأيضًا “بويان سافريتش “Bojan Savric، إلى إظهار الدول المتقدمة في الشمال وكذلك الدول النامية في الجنوب، بما فيها الدول الإفريقية، بأحجام مُتناسبة تعكس حجمها في الواقع دون تشوُّهات، من خلال إبراز الخطوط العريضة للقارات بطريقة بصرية جذابة ومتوازنة1.
10Lengo la Mchoro wa Dunia Iliyolingana (The Equal Earth Projection), ambao ni aina ya mchoro wenye umbo la nusu-silinda uliotengenezwa mwaka 2018 na Bernhard Jenny kutoka Chuo Kikuu cha Monash nchini Australia, Tom Patterson kutoka Huduma ya Hifadhi za Taifa ya Marekani, pamoja na Bojan Savric, ni kuonyesha nchi zilizoendelea za Kaskazini pamoja na nchi zinazoendelea za Kusini, zikiwemo nchi za Afrika, kwa ukubwa unaolingana na ukubwa wao halisi bila upotoshaji. Hili hufanyika kwa kuonyesha mipaka na maumbo ya mabara kwa njia ya kuvutia, yenye uwiano na inayoeleweka kwa urahisi.¹
11وقد أعلن الاتحاد الإفريقي دعمه وتأييده الكاملين لاعتماد إسقاط الأرض المتساوية، داعيًا المُنظمات الدولية إلى التخلّي عن خريطة ميركاتور، كما قدَّم طلبًا رسميًّا إلى اللجنة الأممية المعنية بالخرائط (UN-GGIM) التابعة للأمم المُتحدة لاعتماد الخريطة البديلة، من أجل تصحيح الصورة الذهنية العالمية عن إفريقيا.
11Umoja wa Afrika umetangaza kuunga mkono kikamilifu kupitishwa kwa Mchoro wa Dunia Iliyolingana, huku ukizitaka taasisi za kimataifa kuachana na ramani ya Mercator. Aidha, Umoja huo uliwasilisha ombi rasmi kwa Kamati ya Umoja wa Mataifa inayohusika na masuala ya ramani (UN-GGIM), iliyo chini ya Umoja wa Mataifa, ili kupitisha ramani hiyo mbadala kwa lengo la kurekebisha taswira ya kiakili ya Afrika duniani.
12وفي هذا الصدد قالت “سلمى مليكة حدادي”، نائبة رئيس مفوضية الاتحاد الإفريقي: إنَّ الأمر لا يتعلق بمجرد خريطة، بل بصورة ذهنية ترسَّخت لعقود، مؤكدةً دعم الاتحاد الإفريقي لهذه المُبادرة؛ لكونها تتماشى مع هدفه في استعادة إفريقيا لمكانتها المُستحقّة على الساحة الدولية، في ظل تصاعد الدعوات للمطالبة بتعويضات عن الحقبة الاستعمارية والعبودية2.
12Kuhusiana na suala hilo, Salma Malika Haddadi, Naibu Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika, alisema kwamba suala hili halihusu ramani tu, bali linahusu taswira ya kiakili ambayo imejengeka kwa miongo kadhaa. Alisisitiza kwamba Umoja wa Afrika unaunga mkono mpango huu kwa sababu unaendana na lengo lake la kurejesha Afrika katika nafasi yake inayostahili katika medani ya kimataifa, wakati ambapo wito wa kutaka fidia kutokana na kipindi cha ukoloni na utumwa unazidi kuongezeka.²

13ويعكس هذا الموقف إدراك الاتحاد الإفريقي لأهمية الخريطة، ليس لكونها مجرد أداة لتحديد الاتجاهات، بل بوصفها مخطوطة بصرية تصوغ علاقات القوة وتُعيد تشكيل المخيال العالمي، وبالتالي يُمكن قراءة دعم الاتحاد الإفريقي للمطالب الداعية إلى اعتماد إسقاط الأرض المتساوية على أنه خطوة تستهدف إعادة كتابة التاريخ الإفريقي بلغة بصرية جديدة، أملًا في الخروج من إطار التمثيلات النمطية التي تحصر القارة الإفريقية في خانة الفقر والأوبئة والصراعات المُسلَّحة، وإظهار الجوانب الأخرى التي تؤكد قوة القارة الديمغرافية والاقتصادية3.
13Msimamo huu unaonyesha namna Umoja wa Afrika unavyotambua umuhimu wa ramani, si kwa sababu tu ni chombo cha kuonyesha mwelekeo na maeneo, bali pia kama hati ya taswira inayounda mahusiano ya nguvu na kuathiri namna dunia inavyoifikiria. Kwa hiyo, kuungwa mkono na Umoja wa Afrika kwa madai ya kupitishwa kwa Mchoro wa Dunia Iliyolingana kunaweza kutazamwa kama hatua inayolenga kuandika upya historia ya Afrika kwa kutumia lugha mpya ya taswira, kwa matumaini ya kuondokana na mfumo wa taswira potofu unaolifungamanisha bara la Afrika na umaskini, magonjwa ya milipuko na migogoro ya silaha, na badala yake kuonyesha nyanja nyingine zinazosisitiza nguvu ya Afrika katika demografia na uchumi.³
14يُمكن القول: إنَّ محاولة تبنّي أو اعتماد خريطة جديدة تُظهر إفريقيا ودول الجنوب العالمي بحجمها الحقيقي تشكِّل خطوةً رمزيةً لاستعادة الشعوب الإفريقية لمكانتها بين الأمم، فالخريطة التي ينشدها الأفارقة والاتحاد الإفريقي تُمثِّل جزءًا من مطالب استعادة الحقوق ومُعالجة المظالم التاريخية التي تعرَّضت لها دول القارة وشعوبها لأكثر من قرن على يد القوى الأوروبية الاستعمارية، كما أنَّ هذه الخطوة، رغم رمزيتها، يُمكن أنْ تُعزّز شعور الوحدة والانتماء بين أبناء القارة، وتوحي بقدرة إفريقيا على صياغة رؤيتها وبلورة تصوُّراتها حول ذاتها بنفسها، وليس بما يُريده الآخرون لها أو يُصوّرونه عنها.
14Inaweza kusemwa kwamba juhudi za kupitisha au kuidhinisha ramani mpya inayoonyesha Afrika na nchi za Dunia ya Kusini kwa ukubwa wake halisi zinawakilisha hatua ya kiishara ya kurejesha hadhi ya watu wa Afrika miongoni mwa mataifa. Ramani ambayo Waafrika na Umoja wa Afrika wanaitaka ni sehemu ya madai ya kurejeshwa kwa haki na kushughulikiwa kwa dhuluma za kihistoria ambazo nchi na watu wa bara hili walikumbana nazo kwa zaidi ya karne moja mikononi mwa tawala za kikoloni za Ulaya. Aidha, hatua hii, licha ya kuwa ya kiishara, inaweza kuimarisha hisia za umoja na utambulisho miongoni mwa watu wa bara hili, na kuonyesha uwezo wa Afrika wa kujitengenezea maono yake na kuunda mitazamo yake kuhusu yenyewe, badala ya kutegemea yale ambayo wengine wanataka iwe au wanavyoichora na kuielezea.
15فإفريقيا، ليست قارةً مهمَّشةً أو بعيدةً عن مركز الثقل الدولي كما تُظهرها خريطة ميركاتور، بل إن مُعطيات الواقع تشير إلى أنَّ إفريقيا تُعادل في مساحتها أوروبا والولايات المتحدة والصين واليابان مجتمعةً، ويقطنها أكثر من مليار نسمة وتضم بين حدودها 54 دولةً، كما أنها تكتنز في بواطنها الكثير من الثروات والمعادن الإستراتيجية التي تُعزّز موقعها كفاعل مؤثر في السياسات الدولية.
15Afrika si bara lililotengwa au lililo mbali na kitovu cha nguvu za kimataifa kama linavyoonyeshwa na ramani ya Mercator. Kinyume chake, takwimu za hali halisi zinaonyesha kwamba eneo la Afrika ni sawa na jumla ya maeneo ya Ulaya, Marekani, China na Japan kwa pamoja. Bara hili lina wakazi zaidi ya bilioni moja na linajumuisha nchi 54, huku likiwa na utajiri mkubwa wa maliasili na madini ya kimkakati yaliyomo ndani ya ardhi yake, ambayo yanaimarisha nafasi yake kama mshiriki mwenye ushawishi katika siasa za kimataifa.
16ومع ذلك، فإنَّ رحلة البحث عن خريطة جديدة تُعيد لإفريقيا وزنها الحقيقي عالميًّا، تبقى مهمةً شاقةً كونها تُمثل امتدادًا لمعركة أوسع تسعى خلالها القارة إلى تقديم سرديتها الخاصة وإسقاط السردية الاستعمارية التي هيمنت لقرون. لكنّ نجاح إفريقيا في هذه المهمّة سيُعزّز، بلا شك، رصيدها الدبلوماسي والاقتصادي، وهو ما يُمكن توظيفه واستثماره بشكل إيجابي للارتقاء بمكانة القارة الإفريقية بين الأمم4.
16Hata hivyo, safari ya kutafuta ramani mpya itakayoirejeshea Afrika uzito wake halisi duniani bado ni kazi ngumu, kwa kuwa ni sehemu ya mwendelezo wa mapambano mapana zaidi ambayo bara hili linaendelea nayo ili kuwasilisha simulizi yake yenyewe na kuondokana na simulizi ya kikoloni iliyotawala kwa karne nyingi. Lakini mafanikio ya Afrika katika jukumu hili, bila shaka, yataimarisha mtaji wake wa kidiplomasia na kiuchumi, ambao unaweza kutumiwa na kuendelezwa kwa njia chanya ili kuinua hadhi ya bara la Afrika miongoni mwa mataifa.⁴
17في الختام، يُمكن القول بأنَّ دعم الاتحاد الإفريقي لاعتماد خريطة جديدة، تُظهر القارة بحجمها الفعلي؛ يحمل في طياته دلالات سياسية عميقة، فمن ناحية تعكس هذه المُبادرة تأكيد المُنظمة الإقليمية على الاستقلال الإستراتيجي للقارة وتجاوزها لحقبة التبعية السياسية، وتؤكد من ناحية أخرى إمكانية إعادة النقاش حول مسائل كامنة تتعلق بالتعويضات المُستحقة للبلدان الإفريقية عن العبودية والاستعمار؛
17Kwa hitimisho, inaweza kusemwa kwamba kuungwa mkono na Umoja wa Afrika kwa kupitishwa kwa ramani mpya inayoonyesha bara hilo kwa ukubwa wake halisi kuna maana pana za kisiasa. Kwa upande mmoja, mpango huu unaonyesha msisitizo wa taasisi hiyo ya kikanda kuhusu uhuru wa kimkakati wa bara na juhudi zake za kuvuka kipindi cha utegemezi wa kisiasa. Kwa upande mwingine, unafungua tena uwezekano wa mjadala kuhusu masuala yaliyopo kwa muda mrefu yanayohusiana na fidia zinazodaiwa kustahili kutolewa kwa nchi za Afrika kutokana na utumwa na ukoloni.
18إلا أنَّ هذا التوجُّه من جانب الاتحاد الإفريقي يحتاج إلى إرادة سياسية حقيقية لترجمته إلى واقع فِعْلي؛ لأنه من غير المتوَّقع أنْ تستجيب الحكومات أو المُنظمات والتكتلات الدولية، وكذلك وسائل الإعلام العالمية، بسهولةٍ لهذه المُبادرة الساعية لاستبدال خريطة يعود العمل بها إلى عدة قرون بأخرى تم تطويرها قبل بضع سنوات.
18Hata hivyo, mwelekeo huu wa Umoja wa Afrika unahitaji utashi wa kweli wa kisiasa ili kuugeuza kuwa uhalisia. Hii ni kwa sababu si rahisi kutarajia serikali, mashirika na jumuiya za kimataifa, pamoja na vyombo vya habari duniani, kukubali kwa urahisi mpango huu unaolenga kubadilisha ramani ambayo imetumika kwa karne kadhaa na kuweka nyingine ambayo imetengenezwa katika miaka michache iliyopita.


No posts were found for provided query parameters.
Jarida
Barua fupi ya kila mwezi kutoka Afrophilic: maarifa ya soko, mikataba na habari kutoka Tanzania na Afrika Mashariki.
Barua pepe moja kwa mwezi. Jiondoe wakati wowote.

